Robert Habeck kuchaguliwa kukiongoza chama cha Kijani
17 Novemba 2024Matangazo
Hatua hiyo itafikiwa mwishoni mwa kongamano la siku tatu la chama hicho linalomalizika hii leo Jumapili. Waziri wa Uchumi Robert Habeck ana nafasi kubwa kubwa zaidi ya kuchaguliwa kukiongoza chama cha kijani kuliko mpinzani wake mkubwa Waziri wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock, aliyegombea ukansela kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2021.
Soma Pia: Mkwamo wa bajeti watishia kuivunja serikali ya Ujerumani
Baerbock alisema mnamo mwezi Septemba kwamba safari hii hatagombea. Robert Habeck, ambaye pia ni makamu wa kansela katika serikali ya Kansela Olaf Scholz wiki hii alithibitisha mipango yake ya kugombea nafasi hiyo ya juu.