Tumeimarisha mfumo wa haki jinai na madai-Rais Samia
1 Februari 2024Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini Tanzania kilichofanyika jijini Dodoma yaliyopo makao makuu ya chama na serikali.
Akihutubia katika kilele cha maadhimisho hayo, Rais Samia amesema kuwa malalamiko yamekuwa mengi katika kila pembe huku wananchi wakiwa na uhitaji mkubwa wa msaada wa kisheria hususani katika maeneo ya ardhi, matuzo ya watoto, ndoa ,mirathi, ukatili wa kijinsia na madai kwa mujibu wa taarifa iliyobainishwa na kampeni maalumu ya msaada wa kisheria wa mama Samia iliyoanzishwa kwa ajili ya kufuatilia masuala ya kisheria kwa wananchi.
Rais Samia ameongeza kusema kuwa, serikali iliamua kufanya kampeni hiyo na kwamba, kampeni hiyo imepokelewa vyema na wananchi na katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Shinyanga, Ruvuma, Singida pamoja na Simiyu.
Soma pia:Hali ya haki za binadamu Afrika hairidhishi
Ameitaka wizara ya sheria na katiba kuhakikisha inashirikiana na wadau, katika kuimarisha suala zima la utolewaji wa haki katika maeneo hayo.
"Sasa nitake wizara ya katiba na sheria kushirikiana na wadau, kutekeleza kamilifu mfumo wa utolewaji wa msaada wakisheria," alisema rais Samia.
Ameongeza kwamba kutekelezwa kwa mfumo huo ipasavyo ni uwekezaji mkubwa katika masuala mazima ya haki za binadamu.
Kasoro katika mifumo ya utolewaji haki
Mbali na hayo, Rais Samia amesema kuwa jitihada kubwa zimefanyika kwa lengo la kuimarisha mfumo wa haki jinai nchini Tanzania lakini akagusia suala la mfumo wa haki madai.
" Mfumo wa haki madai na kwenyewe pia kuna malalamiko, kesi zinacheleweshwa, mzunguuko ni mkubwa," alisema rais samia katika maadhimisho hayo."
Wakati Tanzania ikiadhimisha kilele cha wiki ya sheria wananchi katika maeneo mbalimbali nchini humo, wamekuwa na maoni mseto kuhusiana na maadhimisho hayo.
" Kumekuwa na delaying kubwa kwenye maamuzi yanayotolewa kwenye baraza la ardhi, hasa kwenye ngazi ya juu, kwa sababu ile delaying inaweza kupelekea watu wakakosa haki zao au wakakata tamaa kufuatilia shauri lao." Mkaazi wa Dodoma bwana Omary Mohamed, aliiambia DW.
Soma pia:Utafiti: Idadi ya wanawake wanaouwawa yaongezeka Tanzania
Kilele cha maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Chinangali jiji Dodoma, huku kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ikiwa ni umuhimu wa dhana ya haki kwa usitawi wa taifa, nafasi ya mahakama na wadau katika kubolesha mfumo jumuishi wa haki jinai.
Kilele cha maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Chinangali jiji Dodoma, huku kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ikiwa ni umuhimu wa dhana ya haki kwa usitawi wa taifa, nafasi ya mahakama na wadau katika kubolesha mfumo jumuishi wa haki jinai.