Seoul: Urusi iliipa Korea Kaskazini mifumo ya ulinzi wa anga
22 Novemba 2024Shin, amesema hayo katika kipindi cha televesheni cha kituo cha SBS na kuongeza kuwa Korea Kusini imegundua kuwa Urusi ilipokea si tu makombora bali pia vifaa vingine vya kuimarisha ulinzi wake wa anga katika mji mkuu Korea Kaskazini, Pyongyang.
Shin pia amesema Urusi ilitoa msaada wa kiuchumi kwa Korea Kaskazini pamoja na teknolojia mbali mbali za kijeshi zinazojumuisha zile zinazohitajika kusaidia Pyongyang kutengeneza mfumo wa kutegemewa wa ulinzi wa anga.
Soma zaidi:
Marekani, KoreaKorea Kaskazini yaidhinisha mkataba wa kihistoria wa ulinzi na Urusi Kusini na Ukraine zinasema Korea Kaskazini ilituma zaidi ya wanajeshi 10,000 kwenda Urusi mnamo mwezi Oktoba, ambao baadhi yao wanadaiwa kuanza kutumika katika mapambano.
Hayo yanajiri wakati Rais Vladimir Putin akisema kuwa vita vya Ukraine vinageuka kuwa mgogoro wa kidunia. Hii ni baada ya Marekani na Uingereza kuiruhusu Ukraine kuishambulia Urusi na silaha inazopewa na nchi hizo. Putin amezionya nchi za Magharibi kuwa Moscow inaweza kujibu mashambulizi hayo.