Serikali ya Taliban yawazuia wasichana kurudi shule
23 Machi 2022Kundi la Taliban nchini Afghanistan limebadili msimamo kuhusu tangazo lake la kuruhusu shule za wasichana kufunguliwa.Leo Jumatano kundi hilo limesema zitaendelea kufungwa mpaka pale utakapotengenezwa mfumo utakaokwenda sambamba na sheria za kiislamu katika shule hizo za wasichana.
Wizara ya elimu nchini Afghanistan wiki iliyopita ilitangaza kwamba shule zote ikiwemo zile za wasichana kote nchini zitafunguliwa tena leo Jumatano na kuanza kutowa mafunzo ikiwa ni baada ya miezi chungunzima ya kufungwa shule za elimu ya juu za wasichana.
Walimu na wanafunzi kutoka shule tatu za sekondari zilizopo katika mji mkuu Kabul wamesema wasichana walifika shule kwa hamasa na furaha nyingi hii leo asubuhi lakini wakaamrishwa warudi majumbani kwao. Na imeelezwa wengi walirudi majumbani huku wakibubujikwa machozi.
Mwanafunzi mmoja aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwasababu za kiusalama amesimulia namna alivyovunjika moyo na kukosa matumaini kabisa baada ya mkuu wa shule kuwataka warudi nyumbani, mwanafunzi huyo anasema hata mkuu wa shule mwenyewe alikuwa akibubujikwa machozi.
Jumuiya ya Kimataiafa iliweka sharti la watoto wakike kuruhusiwa kwenda shule kuwa moja ya mapendekezo muhimu yatakayotowa uwezekano wa serikali ya Taliban kutambuliwa kimataifa. Umoja wa Mataifa na Marekani zimeilaani hatua hii iliyochukuliwa leo na Taliban.
Jana Jumanne jioni wizara ya elimu ilitowa mkanda wa vidio ikimuonesha msemaji wa wizara hiyo akiwapongeza wanafunzi wote akiwatakia kheri wakati leo watakaporejea kwenye masomo yao. Ghafla hii leo wizara hiyo imebadili mwelekeo na kutangaza kwamba shule za wasichana hazitofunguliwa mpaka pale utaratibu utakaokwenda sambamba na sheria za kiislamu na utamaduni wa Kiaafghani utakapowekwa.
Kundi la Taliban lililotwaa madaraka kwa nguvu mnamo mwezi Agosti mwaka jana, liliwahi huko nyuma kuitawala Afghanistan kuanzia mwaka 1996 mpaka 2001 walipiga marufuku shule zote zinazotowa elimu kwa wanawake na wasichana pamoja na kuwazuia kufanya kazi.
Msemaji wa wizara ya elimu hakupokea simu wala kujibu ujumbe wowote uliomtaka atowe tamko kuhusu taarifa ya wasichana wanaosoma elimu ya juu kuzuiwa kwenda shule hii leo ingawa duru za serikali zimelithibitishia shirika la habari la Reuters kwamba shule za wasichana za mjini Kabul zitaendelea kufungwa kwa sasa,japo hakuna ufafanuzi zaidi uliotolewa.
Mjumbe wa Marekani kuhusu Afghanistan Ian McCary aliyeko Qatar kwa sasa amesema kitendo cha Taliban kinavunja