Sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki zaibua utata
28 Julai 2024Baadhi ya makundi ya Kikatoliki na maaskofu wa Ufaransa wamelaani kile walichokiona kama "matukio ya kejeli dhidi ya Ukristo" katika gwaride la Ijumaa lililoandaliwa na muongozaji filamu Thomas Jolly.
Soma pia:Paris yanga'a katika sherehe ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki
Ukosoaji huo umelenga tukio linalohusisha wacheza densi, wanaume waliovalia kike ili kutumbuiza na mchezaji muziki wakiwa katika hali zilizoibua kumbukumbu za Alhamisi kuu, mlo wa mwisho unaosemekana Yesu alikula na mitume wake.
Hakukuwa na nia ya kutoheshimu kundi lolote la kidini
Msemaji wa michezo hiyo ya olmpiki ya mwaka 2024 Anne Descamps, amewaambia waandishi habari leo kwamba ni wazi hakukuwa na nia ya kutoheshimu kundi lolote la kidini.
Descamps ameongeza kusema ikiwa kuna watu waliokwazika, wanaomba radhi.