Somalia: Puntland kutotambua taasisi za serikali
1 Aprili 2024Serikali ya Puntland inataka kura kamili ya maoni kuhusu mabadiliko yaliopangwa kufanyiwa katiba ya nchi hiyo.
Mabadiliko ya katiba yalioidhinishwa
Siku ya Jumamosi, Rais wa Somalia aliidhinisha mabadiliko kadhaa ya kikatiba. Mabadiliko hayo ni pamoja na mfumo wa kura moja kwa mtu mmoja, kuanzishwa kwa chaguzi za moja kwa moja za urais na kumruhusu Rais kumteuwa waziri mkuu bila ya idhini ya bunge.
Soma pia:Viongozi wa majimbo wataka kumalizwa kwa mgogoro wa kimamlaka Somalia
Kwasasa, Somalia inatumia mfumo tata wa upigaji kura usio wa moja kwa moja unaozingatia koo ambao umekuwa ukitumika kwa zaidi ya nusu karne.
Soma pia:Puntland yasitisha uhusiano wake na serikali ya Somalia
Mfumo huo umesababisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na hujuma za makundi ya wanamgambo kama vile al-Shabab.
Mipango hiyo mipya imekosolewa na kutajwa kuipa serikali kuu uwezo mkubwa.