Somalia yatumbukia kwenye mgogoro mpya
9 Septemba 2021Matangazo
Hali hiyo imeitumbukiza nchi katika mgogoro mkubwa wa kisiasa. Waziri Mkuu wa Somalia Mohammed Hussein Roble amemtuhumu rais wa nchi hiyo Mohammed Abdullahi Mohammed kwa kuingilia kati uchunguzi kuhusu hatima ya wakala mmoja wa idara ya ujasusi ambaye kutoweka kwake kumeibua ukosoaji mkubwa nchini humo.
Bi Ikran Tahlil aliyekuwa na umri wa miaka 25 alitekwa nyara karibu na makazi yake mjini Mogadishu mwezi Juni, na wiki iliyopita waajiri wake waliamua baada ya kufanya tathmini kwamba alitekwa na kuuliwa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.
Rais Mohammed amemteua mkuu mpya wa idara ya ujasusi hatua ambayo inazidisha mvutano kati yake na waziri mkuu ambaye alikuwa amemteua mtu mwingine kushika nafasi hiyo.