Sonko awahimiza Wasenegal kujitokeza kabla ya hotuba ya rais
3 Julai 2023Sonko ameandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa lazima Wasenegal wajitokeze kupambana na utawala wa Macky Sall na kumwambia kuwa hana dhamana ya kuwachagua wagombea watakaoshindana katika uchaguzi ujao wa rais.
Sonko alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mwezi uliopita kwa kumpotosha mwanamke, uamuzi uliozusha maandamano yaliyosababisha vifo vya watu 16.
Hukumu hiyo inamzuia kugombea katika uchaguzi wa rais wa mwaka ujao. Amefungiwa nyumbani kwake tangu Mei 28.
Sall, anatarajiwa kutangaza leo usiku kama atawania au la. Alichaguliwa mara ya kwanza 2012 na tena 2019.
Soma zaidi: Sonko awataka Wasenegal kujitokeza kwa wingi kabla ya hotuba ya rais
Katiba inasema rais hawezi kuhudumu kwa zaidi ya mihula miwili, lakini wafuasi wake wanataka agombee tena wakihoji kuwa marekebisho ya katiba katika mwaka wa 2016 yalianzisha upya sheria hiyo.