Spika wa Madagascar asema nchi imo kwenye mkwamo
18 Oktoba 2023Matangazo
Razanamahasoa amewaambia wabunge wa upinzani kwamba Madagascar iko katika hali mbaya, watu wanateseka na wabunge ndio waliosababisha hali hiyo.
Spika huyo ameahidi kufanya kila analoweza kutafuta njia ya kuutanzua mgogoro uliopo kwa maslahi ya taifa.
Wabunge walimshangilia huku wale walio karibu na rais Andrey Rajoelina pia wakihimiza maridhiano.
Hapo jana wabunge wa upinzani walibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kumtaka Waziri Mkuu Christan Ntsay ajiuzulu.
Soma zaidi: EU, Marekani zashitushwa na uvunjaji wa haki Madagascar
Ntsay, mshirika wa Rajoelina ni mkuu wa serikali mpaka mkuu mpya wa dola atakapochaguliwa.
Nafasi hiyo kimsingi inatakiwa kushikiliwa na rais wa baraza la seneti ambaye alikataa kwa sababu za kibinafsi.