Sudan Kusini yazindua mfumo wa kutumia simu kutuma pesa.
26 Septemba 2019Sudan Kusini imezindua mfumo wa kutuma na kupokea pesa kwa kutumia simu katika juhudi za kuimarisha uchumi wa nchi hiyo baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda wa miaka mitano vilivyosababisha vifo vya takriban watu laki nne.
Lakini itabidi changamoto nyingi zishughulikiwe kabla ya huduma hiyo kuenezwa ikiwa ni pamoja na viwango vya juu vya hali ya kutoweza kuandika na kusoma na ukosefu wa vitambulisho vinavyohitajika kuwasajili watu kutumia huduma hiyo.
Katika wiki za hivi karibuni, barabara za mji mkuu wa Juba zimegubikwa na matangazo ya kibiashara ya kuwahimiza watu kusajili katika huduma hiyo.
Kampuni hiyo zinawategemea watu ambao tayari wameshatumia mfumo huo katika mataifa jirani kama Kenya na Uganda kuwashawishi wakaazi wanaotilia shaka huduma hiyo kwamba ni chagua salama zaidi la kifedha kuliko kubeba pesa taslimu.